Posts

Showing posts from May, 2025

HISTORIA YA MAREHEM SHEKH MUHAMMAD MUSSA MZIMBIRI (1959 - 2020)

Image
Àalim Rabbani, Mlezi wa Maadili, Mwanga na Fakhari ya Milima ya Usambara 1.UTANGULIZI; Takriban Miaka 65 iliyopita Katika milima yenye hewa nzuri na mandhari tulivu ya kuvutia ya Usambara, kijiji cha Tema kitongoji cha kwekele kilishuhudia kuzaliwa kwa nuru ya elimu na hekima ambayo ni Sheikh Muhammad bin Mussa Mzimbiri, mmoja wa wanazuoni maarufu wa Milima ya Usambara, Wilaya ya Lushoto Tanga Tanzania aliyetoa maisha yake yote kwa ajili ya Kumtumikia Allah(S.Wt) akiutumikia Uislamu, kusambaza Elimu na kulea jamii kwa maneno na vitendo. Alikuwa alama ya taq'wa, maarifa, na unyenyekevu wa hali ya juu. 2.JINA LAKE NA NASABA YAKE; Jina lake kamili ni: Sheikh Muhammad bin Mussa bin Mzimbiri bin Mpemba bin Kimweri bin Mbega Al-Kindiyy At-Tamtiyy Nasabu yake alitokana na ukoo mashuhuri wa viongozi wa kimila na kidini katika milima ya Usambara. Baba yake Sheikh Mussa Mzimbiri Mpemba, alikuwa miongoni mwa machifu maarufu wa eneo hilo, aliyejulikana kwa uadilifu na uchamungu wake...