WANAUME WENGI WAKIJA KUFANIKIWA HUBADILIKA NA KUNYANYASA WAKE ZAO
Mzee Mmoja anasimulia kisa cha kweli; Binti yangu alikasirikiana na mume wake, akarudi nyumbani kwangu na mtoto wake mdogo wa kike. Kila mara alipokuwa akiondoka kwa mumewe, nakurudi nyumbani nilikuwa namwambia: "Haiwezekani uache nyumba yako," kisha namrudisha. Lakini safari hii hakutaka kurudi kabisa. Aliponiambia kilichotokea, nilielewa kuwa kosa lilikuwa la mkwe wangu. Nikamuambia: "Sawa mwanangu, bado ni mume wako na baba wa mtoto wako, nitakurudisha mwenyewe kwake," Hata ingawa hakuwahi hata kupiga simu kuulizia angalau hali ya mtoto wake. Nikambeba binti yangu na tukaenda kwa mume wake. Tulipofika Yeye akatangulia mbele akagonga mlango nikiwa mimi nimebaki nyuma. Mume wake alipofungua mlango, moja kwa moja akamwambia: "Kama wazazi wako wanaweza kukulisha, kwanini wakurudishe kwangu?" Pale pale niliganda sakafuni, maneno yake yakanichoma kama moto. Akanigeukia kwa mshangao, akaniambia kwa aibu: "Karibu, baba mkwe." Nikajibu: "Wallahi t...