WANAUME WENGI WAKIJA KUFANIKIWA HUBADILIKA NA KUNYANYASA WAKE ZAO


Mzee Mmoja anasimulia kisa cha kweli;

Binti yangu alikasirikiana na mume wake, akarudi nyumbani kwangu na mtoto wake mdogo wa kike. Kila mara alipokuwa akiondoka kwa mumewe, nakurudi nyumbani nilikuwa namwambia:


"Haiwezekani uache nyumba yako," kisha namrudisha.

Lakini safari hii hakutaka kurudi kabisa. Aliponiambia kilichotokea, nilielewa kuwa kosa lilikuwa la mkwe wangu.


Nikamuambia:

"Sawa mwanangu, bado ni mume wako na baba wa mtoto wako, nitakurudisha mwenyewe kwake,"

Hata ingawa hakuwahi hata kupiga simu kuulizia angalau hali ya mtoto wake.


Nikambeba binti yangu na tukaenda kwa mume wake. Tulipofika Yeye akatangulia mbele akagonga mlango nikiwa mimi nimebaki nyuma.


Mume wake alipofungua mlango, moja kwa moja akamwambia:

"Kama wazazi wako wanaweza kukulisha, kwanini wakurudishe kwangu?"


Pale pale niliganda sakafuni, maneno yake yakanichoma kama moto.

Akanigeukia kwa mshangao, akaniambia kwa aibu:

"Karibu, baba mkwe."


Nikajibu:

"Wallahi tunaweza kumlisha,

lakini inaonekana wewe hufai kuwa na mke.

Sasa hivi niko naye na ninamlisha yeye na mtoto wake.

Lakini siku pesa zikiisha, nitakurudishia tena.


Nikamchukua binti yangu tukaondoka, machozi yakitiririka usoni mwangu kwa huzuni.

Kwa sababu heshima na jitihada zetu za kuokoa ndoa ya binti yetu aliziona kama udhaifu na kutoweza.


Nilimwambia binti yangu:

"Nitakata sehemu ya mwili wangu nikulishe wewe na mtoto wako. Usihofu kitu chochote."


Binti yangu akasema:

"Wallahi, baba, kila mara alikuwa akinitukana kwa sababu ya umasikini wetu,

na ingawa aliponioa hakuwa na chochote,

baada ya kupata neema ya Mungu alianza kuniudhi kila siku…

Lakini sikuwahi kuwaambia ili msiumie."


Mimi naingiatu chumbani kwangu nikiwa nimevunjika moyo,

nikaanza kujiuliza kama nilifanya kosa kumrudisha mwanangu nyumbani na kuharibu ndoa ya mwanangu.

Nikaanza kumuomba Mungu amliwaze binti yangu na amchagulie lililo jema.


Siku zikapita, nikahisi kuwa Mungu ananibariki na kunipa riziki.

Mkwe wangu akanipigia simu, akaniuliza:

"Binti yako anarudi lini nyumbani kwake?"


Kila mara nikamjibu:

"Bado naweza kumlisha yeye na binti yako."


Akaanza kunitishia kuwa atampa talaka. Nikamwambia:

"Hiyo siyo hasara."


Subhanallah, nikahisi nguvu.

Nilihisi kuwa Mungu atamtendea haki binti yangu.


Siku moja akamtumia binti yangu barua ya talaka…

Binti yangu aliumia sana kwa ajili ya mtoto wake.

Nikamuambia:

"Mola wako atakuchagulia kilicho bora."


Siku zikaenda, na Mungu akaendelea kunipa riziki.

Kwa sababu binti yangu alikuwa akiomba dua kila wakati:

"Mungu akupe kwa ajili ya mema uliyotutendea."


Nikaanza kuamini kuwa uwepo wa binti yangu ni baraka katika nyumba yangu.

Na kuwa Mungu ananipa riziki kwa sababu yake,

hasa baada ya hali ya aliyekuwa mumewe kudorora baada ya talaka.


Baada ya mwaka mmoja, kijana mwenye maadili na familia nzuri alimposa binti yangu.

Alikubali kulea mtoto wake pia.


Nilifurahi sana kwa sababu Mungu alijibu dua zangu.

Binti yangu akaolewa, miaka ikapita…


Siku moja akarudi nyumbani akiwa amegombana na mume wake mpya.

Aliponiambia kilichotokea, nilielewa kuwa safari hii kosa lilikuwa la binti yangu.

Nikamuambia:

"Twende nikurudishe kwa mumeo."


Nikamsindikiza huku moyo wangu ukidunda…

Niliogopa kusikia maneno kama yale ya zamani.

Nikamuambia binti yangu:

"Nitangulie ukagonge mlango."


Binti yangu akaniangalia na kusema:

"Sawa baba, nitaenda peke yangu."

Lakini nikasisitiza msimamo wangu.


Akapiga hodi, mumewe alipofungua mlango akamwambia:

"Unajua nyumba hii si nzuri bila wewe."

Kisha akaniangalia na kusema:

"Baba mkwe, wewe mwenyewe umemleta...

Wallahi umenitukuza sana."


Pale pale nikaanza kulia, machozi yakitiririka kama mto.

Mkwe wangu akastaajabu, akaniuliza:

"Baba mkwe kuna nini?"


Nikajibu kwa sauti ya kubanwa na maumivu ya furaha:

"Sasa nimepata amani kuhusu binti yangu.

Naweza kufa nikiwa na furaha.

Mungu akupe malipo mema kama ulivyonifariji."


Mafunzo Kutoka Kisa Hiki Cha Kweli:

1. Upendo wa mzazi kwa mtoto hauna kikomo:

Baba huyu alijitoa kwa moyo wote kuhakikisha binti yake anapata heshima, hifadhi na furaha. Alivumilia kudhalilishwa, akahisi maumivu kwa ajili ya mwanawe, lakini hakumuacha.


2. Sio kila ndoa inafaa kuokolewa kwa gharama yoyote:

Wakati mwingine, kubaki kwenye ndoa yenye madhila na dharau siyo hekima. Baba aliona kuwa heshima na amani ya mtoto wake ni bora kuliko ndoa isiyo na utu.


3. Wema hulipwa na Mungu:

Baba alipomchukua binti yake na mjukuu wake, alianza kuona baraka za wazi kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Dua za watoto wanaoishi kwa maumivu lakini bado wanaheshimu wazazi wao huleta baraka kubwa.


4. Usikosee kuonyesha msimamo na kujitetea kwa heshima:

Baba hakupigana au kufoka, bali alijibu kwa busara na msimamo thabiti. Alionyesha kuwa heshima haimaanishi udhaifu.


5. Maamuzi ya wazazi yana athari kubwa katika maisha ya watoto:

Baba alihofia huenda alimharibia maisha binti yake, lakini Mungu alimthibitishia kuwa alichofanya kilikuwa sahihi.


6. Mwenyezi Mungu humtendea haki aliyedhulumiwa:

Hali ya aliyekuwa mkwe wake ilidorora baada ya kumdhalilisha binti wa watu, huku binti na baba yake wakizidi kuinuliwa na Mola.


7. Mwanamume mwema huleta utulivu, si maumivu:

Mume wa pili wa binti alijua thamani ya mkewe na kumheshimu hata alipokosea, tofauti na wa kwanza aliyekuwa dhalimu.


8. Maombi ya watoto wenye uchungu ni yenye nguvu:

Binti alimwombea baba yake kwa dhati, na matokeo yake yalidhihirika kimaisha.


9. Kusamehe na kusaidia sio udhaifu, ni nguvu ya kweli:

Baba hakujibu kwa hasira au visasi, alijibu kwa huruma, msimamo, na dua.


10. Kila majaribu ni mwanzo wa baraka mpya:

Talaka ilimuumiza binti, lakini ikawa mlango wa furaha, heshima na maisha bora zaidi.


Hitimisho:

Hadithi hii ni somo la upendo wa mzazi, heshima ya familia, na jinsi Mungu humuinua anayevumilia na kumtegemea Yeye.

Mwenyezi Mungu atupe busara ya malezi na maamuzi yenye hekima. Na atupe mapenzi ya kuishi na wenza wetu kwa kuwapenda na kuwahurumia Aamin.

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

HISTORIA YA MAREHEM SHEKH MUHAMMAD MUSSA MZIMBIRI (1959 - 2020)