ALIINGIA NGAMIA KWA MTUME(S.A.W)
Aliingia Ngamia kwa Mtume(s.a.w) kana kwamba ngamia huyu anamjua mtume(saw) ngamia yule akaweka mdomo wake juu ya sikio la bwana mtume(saw).
Mtume(saw) akanyamaza akimsikiliza ngamia yule mpaka alipomaliza kumsemesha mtume(saw) kisha Mtume (saw) akasema, nendeni kwa fulani mkamuite aje,
Wale maswahaba wakenda wakaja naye mpaka kwa mtume(saw)
Mtume (saw) akamuuliza yule bwana aliyeenda kuitwa
Je wewe ndiye mwenye ngamia huyu?
Yule mtu akajibu, ndio yaa rasuulallah
Mtume(saw) akamuambia yule bwana, ngamia wako anakushtakia kwa mwenyezimungu kwamba wewe unakuwa mkali kwake na unambebesha mizigo mizito ambayo hawezi kuibeba na hakika ameshakuwa ngamia wako ni mkubwa wa umri(mzee)
Mtume(saw) akamuambia yule bwana
Niuzie huyu ngamia wako
Yule bwana akamuuzia mtume yule ngamia
Mtume(saw) akasema kumuambia ngamia yule,
"Nenda unapotaka kwenda, na tafuta malisho unavyotaka mwenyewe na wala usihuzunike juu ya yaliyokwisha pita.
Baasi ngamia akainama kwenye sikio la mtume(saw) na akamsemesha mtume(saa) kwa lugha ambayo haifahamu lugha hiyo ispokuwa mtume mwenyewe(saw)
Na mtume(saw) akawa anaitika Aamiin Aamiin Aamiin
Na ktk neno la nne akalia sana mtume(saw)
Maswahaba wakamuuliza Mtume(saw) Ewe mtume wa mungu, kwanini uliitika aamiin mara tatu na ukalia mara ya nne?
Akasema Mtume(saw)
Hakika ngamia ameniombea kwa mwenyezimungu akisema
"Akujaze mwenyezimungu Ewe mtume wa qur'an kwangu mimi na uislamu kheri" nikaitikia Aamiin.
Kisha akaomba hali ya kusema,
Allah auepushie umma wako kutokana na aibu za dunia na adhabu za akhera,
Nami nikasema aamiin
Kisha akaniambia
Allah aulinde/austiri umma wako siku ya qiyama kama ulivyo nilinda/nistiri mimi,
Nikasema Aamiin.
Kisha akasema,
Allah asijaalie ubaya wowote kati ya umma wako
Nikalia
Kwasababu ninajua kwamba ubaya wa umma huu utakaokuwa baina yao ni kubwa mno
Ukimaliza kusoma mswalie mtume muhammad swallallahu alayhi wasallama.
Usiache kutufuatilia kwenye ukurasa wetu wa Facebook wa Alfaqeer Sufian Mzimbiri
Comments
Post a Comment