ALIMPA SHEKH WAKE NG'OMBE MARA BAADA YA KUMALIZA JUUZUU AMMA.

ALIMPA SHEKH WAKE NG'OMBE MARA BAADA YA KUMALIZA JUUZUU AMMA.
Mzee Rashid ni mmoja miongoni mwa wanafunzi wa Marhum Shekh Muhammad Mzimbiri. Mzee Rashid licha ya umri wake kuwa mkubwa lakini aliamua kukita goti mbele ya marhum na akaanza kusomeshwa Juuzuu Amma. Mzee Rashid ambaye alisoma Kwa juhudi licha ya umri wake kuwa mkubwa akitembea na bakora Kwa kujipa sapoti lakini aliweza kujikongoja kila siku akitembea umbali wa mita takriban 800m kwenda madrasa na kurudi Mzee Rashid siku aliyo maliza juuzuu Amma na kukabidhiwa Mas'hafu alirudi nyumbani kwake. Siku iliyofuata tukiwa tumekaa nyumbani Kwa Shekh Ghafla anatokea watu wawili wakiwa wanamswaga ng'ombe huyo mkubwa na kufika mpka mbele ya Shekh Walipofika wakamuambia tumeagizwa na Mzee Tukuletee Ng'ombe huyu, na hapo haujapita muda akatokea Mzee Rashid mwenyewe akafika mbele ya Shekh na akamuambia ng'ombe huyu ni kwaajili yako na ni sadaqa yangu Kwa kunisomesha nikaweza kuisoma Qur'an Kwa uzuri kabisa. Shekh Muhammad alikataa zawadi hiyo lakini akaonekanwa Mzee Rashid ameinuiya haswa zawad hiyo na ikampasa Shekh kumpokea Ng'ombe huyo na akamuambea Mzee Dua. Alhamdulillah Leo nimekutana naye akiwa ana Afya njema na akitembea kuelekea kumzika Mama Wa Shekh Almas bin Shekh Nuhu nikapata kukumbuka kipindi cha miaka takriban 10 iliyopita. Namuomba Allah Amhifadhi na Ampe Siha njema Babu yetu Mzee Rashid Kasherente, Aamiin

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA MAREHEM SHEKH MUHAMMAD MUSSA MZIMBIRI (1959 - 2020)

WANAUME WENGI WAKIJA KUFANIKIWA HUBADILIKA NA KUNYANYASA WAKE ZAO