HISTORIA YA CHANZO CHA ADHANA
Adhana ilitokana na NDOTO aliyo oteshwa swahaba Abdullah bin Zaydi,
>
Nikatika mwaka wa kwanza wa hijra ya mtume (s.a.w) kuhamia madina
Siku moja mtume alikaa na maswahaba zake na akawataka ushauri nini wafanye pindi utakapo wadia muda wa swala?
Akashauri mmoja wao, akasema tunyanyue bendera utakapo fika muda wa swala
>
Na mwingine akashauri, tuwashe moto juu ya vichuguu vya milima.
>
Na wengine wakashauri kwamba tupige tarumbeta kama wanavyofanya mayahudi,
>
Na wengine wakasema tugonge kengele kama wafanyavyo manaswara
Na mwingine akashauri kwamba tutumie ulingano,
/>
Baasi mtume hakuafikiana na rai zao wote walioshauri ispokuwa huyu wamwisho aliyesema tutoe ulingano,
p>Baasi akawa sasa mmoja wa aitwaye Abdullah bin Zaydi baina yake na kulala kwake ghafla akamzukia mtu ndotoni akamfundisha ADHANA baasi alipozinduka akampa habari mtume juu ya ndoto yake,
/>
Baasi mtume akamuambia hakika yoo ni ndoto ya kweli,
Baasi Mtume (s.a.w) akamuamrisha Abdullah bin Zaydi amfundishe ADHANA hiyo Bilaali bin Labbaah,
/>
Baasi aliposikia sayyidnaa Umar juu ya ndoto ya Abdullah bin Zaydi Akasema Umar kumuambia bwana mtume (s.a.w) kwamba Wallah (naapa) nimeona ndotoni mfano wa ndoto ya Abdullah bin Zaydi,
Baasi Akazidisha Bilaal ktk swala ya Asubuhi
( الصلاة خير من النوم مرتين)
swala ni bora kuliko usingizi
Na akaliafiki hilo mtume(s.a.w)
/>
Ambalo lengo la ADHANA ni kumzindua aliye ghafilika, na kumkumbusha aliyesahau ili uwe mkusanyiko kwa wote,
Jiunge katika chaneli yetu ya wasapu uweze kusoma visa mbalimbali👇
https://whatsapp.com/channel/0029Va8ZkCJ47XeFAEksBk05
والله أعلم
Naam
ReplyDelete