Posts

WANAUME WENGI WAKIJA KUFANIKIWA HUBADILIKA NA KUNYANYASA WAKE ZAO

Image
Mzee Mmoja anasimulia kisa cha kweli; Binti yangu alikasirikiana na mume wake, akarudi nyumbani kwangu na mtoto wake mdogo wa kike. Kila mara alipokuwa akiondoka kwa mumewe, nakurudi nyumbani nilikuwa namwambia: "Haiwezekani uache nyumba yako," kisha namrudisha. Lakini safari hii hakutaka kurudi kabisa. Aliponiambia kilichotokea, nilielewa kuwa kosa lilikuwa la mkwe wangu. Nikamuambia: "Sawa mwanangu, bado ni mume wako na baba wa mtoto wako, nitakurudisha mwenyewe kwake," Hata ingawa hakuwahi hata kupiga simu kuulizia angalau hali ya mtoto wake. Nikambeba binti yangu na tukaenda kwa mume wake. Tulipofika Yeye akatangulia mbele akagonga mlango nikiwa mimi nimebaki nyuma. Mume wake alipofungua mlango, moja kwa moja akamwambia: "Kama wazazi wako wanaweza kukulisha, kwanini wakurudishe kwangu?" Pale pale niliganda sakafuni, maneno yake yakanichoma kama moto. Akanigeukia kwa mshangao, akaniambia kwa aibu: "Karibu, baba mkwe." Nikajibu: "Wallahi t...

HISTORIA YA MAREHEM SHEKH MUHAMMAD MUSSA MZIMBIRI (1959 - 2020)

Image
Àalim Rabbani, Mlezi wa Maadili, Mwanga na Fakhari ya Milima ya Usambara 1.UTANGULIZI; Takriban Miaka 65 iliyopita Katika milima yenye hewa nzuri na mandhari tulivu ya kuvutia ya Usambara, kijiji cha Tema kitongoji cha kwekele kilishuhudia kuzaliwa kwa nuru ya elimu na hekima ambayo ni Sheikh Muhammad bin Mussa Mzimbiri, mmoja wa wanazuoni maarufu wa Milima ya Usambara, Wilaya ya Lushoto Tanga Tanzania aliyetoa maisha yake yote kwa ajili ya Kumtumikia Allah(S.Wt) akiutumikia Uislamu, kusambaza Elimu na kulea jamii kwa maneno na vitendo. Alikuwa alama ya taq'wa, maarifa, na unyenyekevu wa hali ya juu. 2.JINA LAKE NA NASABA YAKE; Jina lake kamili ni: Sheikh Muhammad bin Mussa bin Mzimbiri bin Mpemba bin Kimweri bin Mbega Al-Kindiyy At-Tamtiyy Nasabu yake alitokana na ukoo mashuhuri wa viongozi wa kimila na kidini katika milima ya Usambara. Baba yake Sheikh Mussa Mzimbiri Mpemba, alikuwa miongoni mwa machifu maarufu wa eneo hilo, aliyejulikana kwa uadilifu na uchamungu wake...

ALIINGIA NGAMIA KWA MTUME(S.A.W)

Aliingia Ngamia kwa Mtume(s.a.w) kana kwamba ngamia huyu anamjua mtume(saw) ngamia yule akaweka mdomo wake juu ya sikio la bwana mtume(saw). Mtume(saw) akanyamaza akimsikiliza ngamia yule mpaka alipomaliza kumsemesha mtume(saw) kisha Mtume (saw) akasema, nendeni kwa fulani mkamuite aje, Wale maswahaba wakenda wakaja naye mpaka kwa mtume(saw) Mtume (saw) akamuuliza yule bwana aliyeenda kuitwa Je wewe ndiye mwenye ngamia huyu? Yule mtu akajibu, ndio yaa rasuulallah Mtume(saw) akamuambia yule bwana, ngamia wako anakushtakia kwa mwenyezimungu kwamba wewe unakuwa mkali kwake na unambebesha mizigo mizito ambayo hawezi kuibeba na hakika ameshakuwa ngamia wako ni mkubwa wa umri(mzee) Mtume(saw) akamuambia yule bwana Niuzie huyu ngamia wako Yule bwana akamuuzia mtume yule ngamia Mtume(saw) akasema kumuambia ngamia yule, "Nenda unapotaka kwenda, na tafuta malisho unavyotaka mwenyewe na wala usihuzunike juu ya yaliyokwisha pita. Baasi ngamia akainama kwenye sikio la mtume(saw) na akam...

HISTORIA YA SAYYID HUSSEIN BADAWY

Image
HISTORIA YA SAYYID HUSSEIN BADAWY Al-habib Al-Alim Al-Fannan Sayyid: Hussein bin Ahmad Al-Badawy Swaleh bin Alwy bin Abdallah bin Hassan Al-Qaadhy bin Ahmad bin Abdallah [Swahib Tuyyur] bin Ahmad bin Harun bin Abdul-Rahman bin Ahmad bin Abdallah bin Shaykh Muhammad Jamali layl bin Hassan Al-Mua’llim bin Muhammad Asadullah Bin Hassan Al-Turaaby bin Ali bin [Faqiihul-Muqaddam] Muhammad bin Ali Ba’alawy bin Muhammad [Swahibul-Mirbat] bin Ali [Khali-Qassam] bin Alwy bin Muhammad [Swahib-Sawma’ah] bin Alwy bin Ubeidillah bin [Al-Imam Al-Muhajir Ila-llahi] Ahmad bin Issa An-Naqib bin Muhammad Jamaludiin bin Ali Al-Ureidhy bin Ja’afar Al-Swadiq bin Muhammad Al-Baqir bin Ali [Zain Al-Abidin] bin Hussein Al-Sibtwy bin Ali bin Abi Twalib,vile vile Hussein Al-Sibtwy bin Fatma Al-Zahra bint Rasuuli llah [S.A.W].( Abu Abdillah) Babake ni: Sayyid Al-Imam Ahmad Al-Badawy bin Al-Habib Swaleh bin Alwy Jamali Layl (Mwenye Badawy) Mamake ni: Bi Qamar bint Muhammad Al-Amoudy Sayyid Hussein alikuwa aki...

ALIMPA SHEKH WAKE NG'OMBE MARA BAADA YA KUMALIZA JUUZUU AMMA.

Image
ALIMPA SHEKH WAKE NG'OMBE MARA BAADA YA KUMALIZA JUUZUU AMMA. Mzee Rashid ni mmoja miongoni mwa wanafunzi wa Marhum Shekh Muhammad Mzimbiri. Mzee Rashid licha ya umri wake kuwa mkubwa lakini aliamua kukita goti mbele ya marhum na akaanza kusomeshwa Juuzuu Amma. Mzee Rashid ambaye alisoma Kwa juhudi licha ya umri wake kuwa mkubwa akitembea na bakora Kwa kujipa sapoti lakini aliweza kujikongoja kila siku akitembea umbali wa mita takriban 800m kwenda madrasa na kurudi Mzee Rashid siku aliyo maliza juuzuu Amma na kukabidhiwa Mas'hafu alirudi nyumbani kwake. Siku iliyofuata tukiwa tumekaa nyumbani Kwa Shekh Ghafla anatokea watu wawili wakiwa wanamswaga ng'ombe huyo mkubwa na kufika mpka mbele ya Shekh Walipofika wakamuambia tumeagizwa na Mzee Tukuletee Ng'ombe huyu, na hapo haujapita muda akatokea Mzee Rashid mwenyewe akafika mbele ya Shekh na akamuambia ng'ombe huyu ni kwaajili yako na ni sadaqa yangu Kwa kunisomesha nikaweza kuisoma Qur'an Kwa uzuri kabis...
atOptions = { 'key' : '8f0fffe407ab1064f7d48a7989ca3385', 'format' : 'iframe', 'height' : 60, 'width' : 468, 'params' : {} }; p> atOptions = { 'key' : '8f0fffe407ab1064f7d48a7989ca3385', 'format' : 'iframe', 'height' : 60, 'width' : 468, 'params' : {} }; ipt> ript> frame allowfullscreen="" class="BLOG_video_class" height="266" src="https://www.youtube.com/embed/PahpMI4ur0M" width="320" youtube-src-id="PahpMI4ur0M">  SWALAATUT TAAJI اللهم صل على سيدنا محمد صاحب التاج...

MTUME ATOA AGIZO BILAL AITWE

Image
  MTUME ATOA AGIZO BILAL AITWE AJE. /> Siku alipofika Bwana Mtume (S.A.W) Makkah kwaajili ya Kuikomboa Makkah (FAT'HU MAKKAH) alisimama Mtume(S.A.W) ktk mlango wa Alkaaba na akauliza "yuko wapi Bilal"? Akasema niitieni Bilaal aje. p> p>Kisha akasema "WALLAHI Enyi maquraysh siachikuwa nimwenye kukumbuka siku ambazo mlikuwa mkiadhibiwa ambapo Bilaal alikuwa akiadhibiwa juu ya mlango huu wa Alkaaba," Naam Bilaal Akaitwa akaja alipofika Bilaal Mtume SAW akamuambia Bilaal, "ingia Ewe Bilaal, Hatoswali na Hatoswali pamoja nami ktk Alkaaba leo hii ispokuwa ww tu Bilaal". /> Na kufanya hivyo ilikuwa ni Takrima na Kumfanya Bilaali ajihisi nayeye ni bora kama wengine na pengine hata kuwazidi wengine, yote hayo ni kwa kumhurumia na kumliwaza juu ya yale aliyapitia baada ya kusilimu ikiwemo kuadhibiwa adhabu kali kupita kiasi pale aliposilimu. /> Na pia ilikuwa ni message nzito kwa waarabu waliodhani mtu mweusi hana haki kama wao na ...