ALIINGIA NGAMIA KWA MTUME(S.A.W)
Aliingia Ngamia kwa Mtume(s.a.w) kana kwamba ngamia huyu anamjua mtume(saw) ngamia yule akaweka mdomo wake juu ya sikio la bwana mtume(saw). Mtume(saw) akanyamaza akimsikiliza ngamia yule mpaka alipomaliza kumsemesha mtume(saw) kisha Mtume (saw) akasema, nendeni kwa fulani mkamuite aje, Wale maswahaba wakenda wakaja naye mpaka kwa mtume(saw) Mtume (saw) akamuuliza yule bwana aliyeenda kuitwa Je wewe ndiye mwenye ngamia huyu? Yule mtu akajibu, ndio yaa rasuulallah Mtume(saw) akamuambia yule bwana, ngamia wako anakushtakia kwa mwenyezimungu kwamba wewe unakuwa mkali kwake na unambebesha mizigo mizito ambayo hawezi kuibeba na hakika ameshakuwa ngamia wako ni mkubwa wa umri(mzee) Mtume(saw) akamuambia yule bwana Niuzie huyu ngamia wako Yule bwana akamuuzia mtume yule ngamia Mtume(saw) akasema kumuambia ngamia yule, "Nenda unapotaka kwenda, na tafuta malisho unavyotaka mwenyewe na wala usihuzunike juu ya yaliyokwisha pita. Baasi ngamia akainama kwenye sikio la mtume(saw) na akam...